Propellerads

Hajji Manara adai anaweza kuiunga mkono Yanga.




Haji Manara, yule mkuu wa kitengo cha habari cha klabu ya Simba, ameweka wazi kwamba anaweza kuiunga mkono Yanga.

Manara ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Yanga, gwiji Sunday Manara ‘Compyuter’ amesema haoni shida kwake kuiunga mkono Yanga licha ya kuwa ni Simba wa kugaragara.

“Inawezekana kabisa kuiunga mkono Yanga kwa maana ya utaifa, au pale wanapokuwa wamefanya jambo zuri ambalo linapaswa kupongezwa.

“Kuiunga Yanga mkono haina maana ya kwamba niwe shabiki wa Yanga, sivyo. Mfano mzuri Yanga walipocheza na timu ya Zimbabwe nilieleza ninavyowaunga mkono.

“Pale lilikuwa ni suala la utaifa, ndiyo maana nikaweka vile ingawa yule jamaa yangu (Jery Muro) alijiudhi sana. Mwisho nikaamua kusema niliyosema,” alisema Manara.


Mambo yanabadilika, lazima tukubali kuna vitu vimepita tunatakiwa kuvifanyia kazi na hasa kuachana na mambo ambayo yamepitwa na wakati.
Hajji Manara adai anaweza kuiunga mkono Yanga. Hajji Manara adai anaweza kuiunga mkono Yanga. Reviewed by Steve on Tuesday, June 23, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.