Wenger: matokeo ya Tottenham ni mazuri

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekipongeza kikosi chake baada ya
sare ya 1-1 na mahasimu wao Tottenham Hotspur hapo jana.
Gunners walijikuta wakitulizwa mapema kipindi cha kwanza kupitia goli la Harry Kane kabla ya Kieran Gibbs kusawazisha huku zikiwa zimesalia dakika 13 mchezo kumalizika.
"Kipindi cha pili tumeonesha nguvu na kikosi kutotaka kupoteza mchezo," Wenger aliiambia BBC Sport "Mwisho nadhani ni vizuri 1-1.
"Mwendo wa Kieran Gibbs ni mzuri. Timing yake kwenye box ni nzuri, muda mwingine anajikuta kwenye nafasi ambayo haamini kama anaweza kufunga.
"Ubingwa unaonesha inatakiwa upambane asilimia 200 kila mchezo."
Arsenal watakutana na West Bromwich na Norwich City katika Premier League kabla ya mapumziko ya kimataifa.
Wenger: matokeo ya Tottenham ni mazuri
Reviewed by Steve
on
Monday, November 09, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, November 09, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment