Kamusoko tayari kwa ajili ya Zanaco daktari athibitisha, kuhusu Mahadhi na Mwashiuya hali ipo namna hii..
Kiungo wa Yanga, Mzimbabwe Thaban Kamusoko sasa
yupo fiti kuivaa Zanaco ya Zambia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa keshokutwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Wakati Kamusoko akirejea uwanjani, Geofrey Mwashiuya na Juma Mahadhi wanaweza kuukosa mchezo huo baada ya juzi kuumia kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Kiluvya United.
Kamusoko aliumia Februari 25 mwaka huu wakati wakicheza na Simba katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa taifa, jijini Dar es Salaam.
Daktari wa timu hiyo, Edward Bavu amesema mchezaji huyo yuko fiti na alianza mazoezi rasmi jana jioni dhidi ya Zanaco.
Buvu alisema wachezaji wengine Mahadhi na Mwashiuya, bado anaendelea kuwafanyia uchunguzi.
Kamusoko tayari kwa ajili ya Zanaco daktari athibitisha, kuhusu Mahadhi na Mwashiuya hali ipo namna hii..
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment