Haya ndiyo maamuzi ya Manyika kwa mwanawe kuongeza mkataba mpya Simba
Kipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Peter Manyika, amesema
atamwondoa mwanawe, Manyika Peter, kudakia Simba kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Joseph Omog.
Peter amesema hatakubali mtoto wake huyo kusaini mkataba mwingine kutokana na kushindwa kutumika katika kikosi cha Simba.
Amefunguka kwamba Manyika na kipa Said Kipao anayeidakia JKT Ruvu ambao walilelewa katika kituo cha 'Tanzania Goalkeeping Training Center (TGTC), hawatasaini mkataba mwingine katika timu hizo.
Alisema atawatafutia timu nyingine za kudakia ili waweze kuendelea timu nyingine za kudakia ili waweze kuendelea kukuza vipaji vyao baada ya kukosa nafasi ya kuonyesha katika timu hizo.
"TGTC tunaamini vijana hawa wana uwezo mkubwa kutokana na mazoezi waliyoyapata kutoka kwetu, hivyo kitendo cha kukosa nafasi katika timu zao ni moja ya sababu ambayo imekuwa ikiwarudisha nyuma," alisema.
Peter alisema Manyika alisainni mkataba wa miaka mitatu katika kikosi cha Msimbazi ambao unatarajiwa kumalizika Juni mwaka huu.
Haya ndiyo maamuzi ya Manyika kwa mwanawe kuongeza mkataba mpya Simba
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment