Kikosi cha Manchester United jana kimepata sare ugenini, Mourinho atoa tathmini ya mchezo
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amefunguka kwamba
ameridhishwa na kiwango cha kikosi chake baada ya mechi ya jana kwenye michuano ya Europa dhidi ya Rostov ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1.
Mourinho amedai kua ilikua ni ngumu kwa kikosi chake kupata matokeo yoyote mazuri kulingana na hali ya uwanja, huku akiridhishwa na kumaliza mchezo bila majeruhi.
"Kilikua ni kiwango kizuri ukilinganisha na hali yenyewe. Isingewezekana kucheza vizuri." aliiambia BT Sport.
"Tulicheza tukiwa na uhitaji na tumecheza vizuri. Tulifanya kosa moja kwenye ulinzi. Tuna matokeo ya wazi mechi ya marudiano huku ikiwa ni nfasi finyu kwetu. Hatuna majeruhi.
"Mawinga hawajatumika sana, mabeki wetu watatu walikua katika hali nzuri kimchezo huku viungo wakipigana kwa ajili ya goli la pili ambapo walijitahidi kusaidia mashambulizi." alisema Mourinho.
Kikosi cha Manchester United jana kimepata sare ugenini, Mourinho atoa tathmini ya mchezo
Reviewed by Steve
on
Friday, March 10, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment