Propellerads

Endapo Ngoma anataka kusepa Yanga, hili ndio jibu pekee kwa sasa...



Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zimeeleza, uongozi wa
Yanga umekubaliana na ombi la Mzimbabwe Donald Ngoma kutaka kuvunja mkataba kwa madai ya kuwa amechoshwa kusakamwa.

Ngoma amekuwa akiwasumbua Yanga kwa madai kuwa ni mgonjwa, lakini taarifa nyingine zikidai alishapona lakini alifanya hivyo kushinikiza katika suala lakuongezewa mkataba mnono.

"Kweli Ngoma alikutana na vice (Makamu mwenyekiti - Clement Sanga). Akamueleza amechoka anataka kuondoka, naye akamuambia aandike barua na aiwasilishe mara moja kuwa anataka kuvunja mkataba.

"Siku iliyofuata, akasisitizwa kuandika barua, hakufanya hivyo. Baada ya hapo, Ngoma mwenyewe tunaona ameanza mazoezi," kilieleza chanzo.

Taarifa nyingi zilizopatikana zilidai kwamba, Sanga alimkemea Ngoma na kumtaka aiheshimu Yanga kwa kuwa ilikuwepo hata kabla ya wazazi wa makamu mwenyekiti na Ngoma mwenyewe.

"Vice alikasirika sana, alimueleza namna alivyoonesha udhaifu kuzozana mitandaoni. Lakini pia alikasirishwa na yule daktari aliyemjibu Ngoma mitandaoni akisisitiza si sahihi kiweledi.

"Tangu Ngoma amesemwa na vice, tunaona ameanza mazoezi na anaonyesha ushirikiano," kilieleza chanzo kingine.

Juhudi za kumpata Sanga zilifanikiwa baada ya kumsaka kwa siku mbili, naye alisema.

"Nafikiri unajua mimi ni kiongozi wa Yanga, kukutana na Ngoma ni jambo la kawaida kabisa. Haitakuwa sahihi kueleza tulizungumza nini kwa kuwa ni mambo ya mzazi na familia yake."
Endapo Ngoma anataka kusepa Yanga, hili ndio jibu pekee kwa sasa... Endapo Ngoma anataka kusepa Yanga, hili ndio jibu pekee kwa sasa... Reviewed by Steve on Friday, March 10, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.