Ngassa kuondoka Mbeya City na kurejea Oman tena, mwenyewe ataja sababu
Mshambuliaji wa Mbeya City, Mrisho Ngassa, amefunguka kuwa
yupo mbioni kuachana na klabu yake ya sasa ya Mbeya City mara baada ya kumalizika mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Ngassa alijiunga na Mbeya City katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Fanja FC ya Oman, amesema mkataba ukiisha amepanga kuondoka kwenda Oman.
"Mkataba niliosaini hapa (Mbeya City) ni wa muda mfupi, hivyo sitaraji kuongeza mwingine. Niliondoka Fanja kwa sababu kibali changu kilikuwa na matatizo na ndiyo maana nikarudi hapa bongo, lakini mipango yangu ikikaa sawa nitarejea kule," alisema Ngassa.
Ngassa kuondoka Mbeya City na kurejea Oman tena, mwenyewe ataja sababu
Reviewed by Steve
on
Friday, March 10, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment