Yanga watuma ujumbe kwa wanaodai wamefulia, ni mwendo wa ndege tu tena 'first class'
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema taarifa zinazotolewa
katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa wana hali mbaya kiuchumi siyo kweli na wamepanga kuthibitisha kwamba wapo vizuri.
Imekuwa ikidaiwa kuwa Yanga haipo vizuri kiuchumi kutokana na mwenyekiti wake, Yusuf Manji kuwa yupo kwenye matatizo binafsi huku kukiwa na matukio kadhaa ya kupunguza matumizi ya klabu na kudaiwa haijawalipa wachezaji wake kadhaa mishahara.
Baada ya taarifa hizo, habari ni kuwa Yanga imesema imeshamalizana na beki wake, Vincent Bossou aliyekua akidai mshahara na aliyekua kocha wao, Ernie Brandits.
Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema watalipa madeni yote wanayodaiwa hivi karibuni kisha usafiri wao wa kwenda kucheza nje kimataifa watakata tiketi za ndege daraja la kwanza 'first class'.
"Wanasema eti tutapanda treni kuelekea Zambia kucheza dhidi ya Zanaco, wanaosema hivyo waambie waje airport siku ya kusafiri washuhudie tutakavyokuwa tukipanda ndege daraja la kwanza," alisema Mkwasa.
Yanga watuma ujumbe kwa wanaodai wamefulia, ni mwendo wa ndege tu tena 'first class'
Reviewed by Steve
on
Friday, March 10, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment