Sanchez avutiwa waya na Man United, Massiliano Allegri kuwa mrithi wa Wenger!?....yote hapa katika tetesi za usajili kutoka magazeti ya Ulaya leo
Klabu ya Manchester United inajipanga kumnasa Alexis Sanchez
kutoka Arsenal kipindi cha majira ya joto.
Arsenal wanaonekana kusuasua katika kumpa mkataba mwingine ambapo inaonekana wazi kwamba raia huyo wa Chile anajiandaa kuondoka na kuelekea klabu nyingine yenye kushinda mataji.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la The Express ni kwamba swala hilo lipo mbioni ambapo kocha Jose Mourinho wa Man United amekua akifatilia kwa karibu ishu ya Sanchez huku Antoine Griezmann ambaye kwa kiwango kikubwa alikua katika hesabu za mashetani hao wekundu akionekana kutaka kuendelea kubaki Hispania.
Ukiacha mbali habari hiyo, hizi hapa pia ni tetesi nyingine za uhamisho kutoka magazeti ya Ulaya siku ya leo Jumamosi:-
- Klabu ya Arsenal wamepewa muda wa wiki tatu kuamua endapo wanahitaji Massimiliano Allegri kuwa mbadala wa kocha Arsene Wenger majira ya joto.
- Liverpool ni miongoni mwa vilabu vikubwa vya Premier League ambavyo vimetuma wasaidizi kumfatilia kwa karibu Moussa Dembele kwenye mchezo kati ya Old Firm na Rangers Jumapili hii.
- Arsenal wanaweza kumsaini nyota wa Juventus, Paulo Dybala endapo Max Allegri akitua kama kocha mpya Emirates, lakini hata hivyo Barcelona na Real Madrid wanamfukuzia nyota huyo.
- LA Galaxy wamefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic kuhusu uhamisho wake kipindi cha majira ya joto, hii ni kwa mujibu wa klabu hiyo ya MLS, Alex Lalas.
- West Bromwich wapo katika mipango ya kumnasa mkongwe wa Chelsea, John Terry, hayo yamethibitishwa na bosi wa klabu hiyo, Tony Pulis.
Sanchez avutiwa waya na Man United, Massiliano Allegri kuwa mrithi wa Wenger!?....yote hapa katika tetesi za usajili kutoka magazeti ya Ulaya leo
Reviewed by Steve
on
Saturday, March 11, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment