Propellerads

Yanga wanacheza na Zanaco leo, Luizio ampa ushauri na mbinu beki wa Yanga, Hassan Kessy



Leo Jumamosi Yanga inatarajiwa kuvaana na Zanaco ya Zambia kwenye
mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, lakini Straika wa Simba, Juma Luizio amempa beki wa Yanga, Hassan Kessy jin la mchezaji hatari wa wapinzani wao.

Huu ni mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi na atakayeondolewa kwenye hatua hii, atashushwa Kombe la shirikisho ambako atatakiwa kucheza mechi mbili za mtoano kabla ya kutinga makundi.

Ikumbukwe Yanga iliiondoa N'gaya ya Comoro kwenye hatua ya awali kwa mabao 6-2 na Zanaco ya Zambia iliiondosha APR ya Rwanda kwa bao 1-0.



Luizio ambaye amewahi kuchezea Zesco ambayo ni wapinzani wa Zanaco amemtaja beki Mzimbabwe, Zimiseleni Moyo 'Rasta' kuwa ndiye amekua mwiba kwa kuanzisha mashambulizi kupitia upande wao wa kulia na kukaba kwa wakati mmoja.

"Ule upande wa kulia, Kessy inabidi acheze kwa umakini mkubwa kwa sababu Zanaco hutumia upande wao wa kushoto kutengeneza mashambulizi yote na hata mabao yao hupatikana huko.

"Nimwambie kwamba, macho na akili yake inatakiwa ielekezwe zaidi kwa Moyo ambaye yeye ni beki lakini anaweza kusaidia kushambulia kwa kiasi kikubwa, pia anakaba na kupiga krosi za hatari zaidi upande wa wapinzni na asilimia kubwa ni vitu ambavyo vimekuwa vikiwasaidia kupata mabao, najua hata Lwandamina (Kocha wa Yanga) anafahamu kuhusu hilo," alisema Luizio.
Yanga wanacheza na Zanaco leo, Luizio ampa ushauri na mbinu beki wa Yanga, Hassan Kessy Yanga wanacheza na Zanaco leo, Luizio ampa ushauri na mbinu beki wa Yanga, Hassan Kessy Reviewed by Steve on Saturday, March 11, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.