Giggs nae aamua kumtetea Pogba kwa hili...
Ryan Giggs amewaambia wote wanaomkosoa Paul Pogba na
kumlalamikia wafyate midomo yao.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa ameshindwa kuonesha ubora uliotarajiwa na wengi kutokana na bei kubwa iliyotumika kumnunua kutoka Juventus kwa pauni mil 89 mwaka jana.
Pogba mpaka sasa ameifungia Manchester United mabao saba katika mechi za mashindano yote huku akitoa assists nne, lakini Giggs ametetea kiwango cha nyota huyo kwa kudai kwamba hakuna mchezaji aliyepata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa umri kama wa Pogba.
"Sijawahi kuona kiungo mwenye umri wa miaka 23 akitawaka michezo kwa msimu mzima, kwa hiyo bei ya pauni mil 90 ni sawa," alisema Giggs kama alivyonukuliwa na Sky Sports.
"Atakuja kua mchezaji mzuri sana, hilo halina shaka. Amefunga magoli saba- sio viungo wengi wenye umri kama wake wanaweza kufanya hilo, lakini kwa vile alinunuliwa bei kubwa anafananishwa na bei yake, akifanya vizuri msimu huu japo sio sana sio mbaya sana,"
Wiki hii pia Pogba amekingiwa kifua na mkongwe mwingine wa United Paul Scholes na anatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa ligi ya Europa dhidi ya Rostov Alhamisi hii.
Giggs nae aamua kumtetea Pogba kwa hili...
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment