Wenger afichua kwanini aliamua kumtoa Santi Cazorla

Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger amefichua kua aliamua
kumtoa Santi Cazorla kwenye mechi waliyotoa sare ya 1-1 na Tottenham Hotspur jana kwa sababu mchezaji huyo alikua na kizunguzungu.

Kiungo huyo Mhispania nafasi yake ilichukuliwa na Mathieu Flamini wakati wa mapumziko kwa maamuzi ya kushtukiza ya Wenger, hata hivyo kocha huyo amesema mabadiliko hayakua ya kiufundi.
"Nilikua nimekaa pale nafikiria, nimtoe au nimuache? Huwezi jua, labda itakua sawa," aliiambia Sky Sports News "Wakati wa mapumziko, nikamtoa, na katika kipindi cha pili tukapata balance kidogo."
"Sio mgonjwa. Alikua na kizunguzungu na hakuweza hata kusogea, ungeweza kuliona hilo uwanjani. Cazorla, ambaye hua ni kiongozi wetu uwanjani, hakupata mpira.
"Nina imani hakuna kibaya, lakini ilionekana kama hivyo, kwa sababu anasema sasa yuko sawa."
Wenger afichua kwanini aliamua kumtoa Santi Cazorla
Reviewed by Steve
on
Monday, November 09, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, November 09, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment