Real Madrid waamua kwa Dyabala, Wilshere nae aweka wazi hatima yake Arsenal....hizi hapa headlines magazeti ya Ulaya leo
Inaonekana kwamba Real Madrid wanamhitaji kwa
kiasi kikubwa Paulo Dyabala ambapo inadaiwa kwa sasa wapo tayari kuwaachia viungo wao Isco na Mateo Kovacic kwenda Juventus ili tu kumnasa mshambuliaji huyo.
Katika magazeti ya Ulaya leo Jumatatu hizi hapa habari nyingine zilizotawala sana
- Chelsea wana matumaini makubwa kukamilisha dili ya makinda wanaokuwa kwa kasi Billy Gilmour na Daishawn Redan.
- Jack Wilshere hafikirii zaidi kuhusu hatima yake klabuni Arsenal.
- Pep Guardiola anaamini kwamba Yaya Toure anaweza kutimkia popote pale atakapohitaji kuelekea.
- Arsenal na Chelsea wanamfatilia kwa karibu nyota Mreno anayekipiga Wolves, Helder Costa.
- Jose Mourinho amekiri kwamba alijua kwamba Marcus Rashford angeweza kusuasua msimu huu, lakini bado ana nafasi nzuri ya kuendelea kucheza.
- Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amedai kwamba Man United wasisingizie michuano ya Europa endapo wakipoteza mechi yao na Chelsea.
- Petr Cech amkingia kifua Alexis Sanchez ambapo amedai picha iliyomuonesha akicheka benchini ilieleweka vibaya kwani haikuwa hivyo.
- Huenda Bayern Munich wakafanya uhamisho wa kushtukiza kwa Granit Xhaka baada ya kuwa katika wakati mgumu Arsenal.
Real Madrid waamua kwa Dyabala, Wilshere nae aweka wazi hatima yake Arsenal....hizi hapa headlines magazeti ya Ulaya leo
Reviewed by Steve
on
Monday, March 13, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment