Propellerads

Conte atoa tathmini yake kwa wanaowafananisha Kante na Pogba




Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amefafanua kwanini
huwezi kuwafananisha N'Golo Kante na nyota wa Manchester United, Paul Pogba.

Kocha huyo Muitaliano, amewahi kufanya kazi na Pogba walipokuwa wote Serie A katika klabu ya Juventus ambapo walishinda mataji kadhaa.

Tangu atue Chelsea, Kante amekua katika kiwango kizuri huku Pogba akijikuta akikosolewa sana msimu huu alipojiunga na Manchester United.

"Ni wachezaji wawili tofauti wakiwa na sifa tofauti," alisema Conte.

"Nilipata nafasi ya kumfundisha Paulo, kwa miaka kadhaa. Tunazungumzia kuhusu mchezaji mkubwa- mkubwa katika kila hali, hati kujituma kwake katika mazoezi.

"Siku zote anajitahidi kua bora, anambinu nzuri, ana nguvu, ana stamina. Tunazungumzia mchezaji mkubwa."


Conte atoa tathmini yake kwa wanaowafananisha Kante na Pogba Conte atoa tathmini yake kwa wanaowafananisha Kante na Pogba Reviewed by Steve on Sunday, March 12, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.