Zanaco walia kufanyiwa figisu na Yanga, soma zaidi hapa kuhusu madai yao
Timu ya Zanaco imelalamikia kufanyiwa vitendo ambavyo
sio vya kiungwana 'figisu' kabla ya mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Yanga.
Meneja wa timu hiyo Stafford Kayame ameituhumu Yanga kupuliza dawa yenye kemikali kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo.
“Kabla ya game chumba kilikuwa hakikaliki, kulikuwa na harufu ya dawa yenye kemikali ambayo ilipulizwa kwenye chumba chetu, kwa hiyo tukaomba kubadilishiwa chumba tulichopewa kwa ajili ya kubadilishia nguo.”
“Tulitoa taarifa kwa match commissioner na kila anayehusika. Daktari wetu alithibisha kuwa kulikuwa na dawa iliyopulizwa kwenye chumba chetu na ingeweza kuwaathiri wachezaji.”
Zanaco walia kufanyiwa figisu na Yanga, soma zaidi hapa kuhusu madai yao
Reviewed by Steve
on
Sunday, March 12, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment