Klopp amegusia uhasama wake na Mourinho

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amedokeza kuhusiana na
uhasama wake na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho.
Mameneja hao wote wawili wameshakutana mara nne kabla, katika michezo kati ya vilabu vyao vya zamani Real Madrid na Borussia Dortmund katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Klopp amesisitiza kua yeye na Mourinho wana uhusiano mzuri na anamheshimu sana kocha huyo Mreno.
"Ninaheshimu sana kazi yake," aliongea na waandishi wa habari kabla ya mechi kwa mujibu Daily Mirror.
"Kama wewe sio mwamuzi au mwandishi, anaweza kua mtu mzuri
"Wakati wa mchezo, wote tunakua na hisia zaidi, lakini ni wataalamu, kila kitu kiko sawa kati yetu.
"Nilipokua Ujerumani, Mourinho na mimi muda mwingine tulitumiana meseji. Ninaheshimu kazi yake. Ni mtu mzuri."
Liverpool na Chelsea wataumana na wikiendi hii katika mchezo wa Premier League.
Klopp amegusia uhasama wake na Mourinho
Reviewed by Steve
on
Friday, October 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, October 30, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment