Ukweli wa Ronaldo kuhusu uhusiano wake na Messi

Cristiano Ronaldo amezungumzia uhusiano wake na Lionel Messi ambapo nyota
huyo Mreno ametoa mtazamo wake.
Wawili hao wameutawala ulimwengu wa soka kwa miaka ya hivi karibuni na inaelekea uhasimu wao unaweza kuwekwa katika vitabu vya historia ya mchezo huo.
Ronaldo hata hivyo amesisitiza kua wote wawili wanapata kitu kutoka kati yao na hamna cha zaidi.
"Namtizama (Mesi), sio kama adui, lakini ni kama mtu anaenifanya mimi kua mchezaji bora na ninamfanya na yeye kua mchezaji bora," amesema katika sehemu ya filamu yake ya Ronaldo:The Movie.
Wote wanaonekana kuheshimiana kwa hali ya juu na uhasimu wao unaonekana sio kwa ubaya lakini unalazimishwa na wengi kua hivyo.
Ukweli wa Ronaldo kuhusu uhusiano wake na Messi
Reviewed by Steve
on
Friday, October 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, October 30, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment