Van Gaal ameamua kumjibu hivi Paul Scholes

Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal ameyatolea nje
madai ya Paul Scholes kwamba timu inakosa ubunifu.
Mkongwe huyo wa Red Devils, alimkosoa kocha huyo na kusema asingeweza kuchezea kikosi kilicho chini yake.
Van Gaal ambaye alichukua jukumu la kuinoa United majira ya joto 2014, ameiwezesha timu kushinda mechi sita kati ya 10 za Premier League msimu huu, lakini ameshindwa kushinda kwenye mechi mbili zilizopita katika michuano yote.
Jumatano, Man United walitolewa Capital One Cup na Middlesbrough wakiwa wamefikia mzunguko wa nne ambapo walipoteza kwa matuta.
Alipoulizwa kuhusu shutuma za Scholes katika mkutano na waandishi wa habari leo, Van Gaal alisema "(Scholes) hana hili jukumu, kwa hiyo anaweza kusema chochote. Kwanini anasema chochote? kwa manufaa ya klabu au kwake?
"Sitaki kujitetea kwa sababu siwezi kutetea, kwa sababu yeye ni mkongwe na ana sauti kubwa, kwa hiyo nasikia. Nadhani unapokua mkongwe, unatakiwa uongee na meneja au rafiki yake Ryan Giigs au Ed Woodward, lakini sio namna hii, kwa sababu atalipwa na BBC au Sky."
"Unaweza kujieleza, fimbo na mawe zinaweza kuvunja mifupa yangu, lakini maneno hayawezi kuniumiza"
United kwa sasa wapo nafasi ya nne katika msimamo wa Premier League wakiwa nyuma kwa point mbili kwa vinara Man City.
Van Gaal ameamua kumjibu hivi Paul Scholes
Reviewed by Steve
on
Friday, October 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, October 30, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment