Propellerads

Jahazi la Tanzania katika soka linazidi kuzama, nani wa kuliokoa!!




Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imezidi kushuka katika viwango vya ubora wa
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ambapo imeshuka kwa nafasi moja zaidi na sasa inashika nafasi ya 140.

Orodha hiyo iliyotolewa jana imeonyesha kuwa, Tanzania ndiyo nchi inayoshika nafasi ya chini zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Uganda inashika nafasi ya 74, Kenya ikiwa ya 116.

Algeria ndiyo inayoongoza kwa Afrika kwa kuwa inashika nafasi ya 19 ikifuatiwa na Ivory Coast inayoshika nafasi ya 21.

Timu zinazoongoza katika 10 bora ni; Argentina, Ubelgiji, Ujerumani, Colombia, Brazil, Ureno, Romania, England, Wales na Chile.
Jahazi la Tanzania katika soka linazidi kuzama, nani wa kuliokoa!! Jahazi la Tanzania katika soka linazidi kuzama, nani wa kuliokoa!! Reviewed by Steve on Friday, August 07, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.