Propellerads

Sababu tatu zinazoweza kumfanya Messi kuondoka Barcelona

                      Lionel Messi
Ripoti huko England zimemhusisha nyota wa FC Barcelona, Lionel Messi kutaka
kuhamia Manchester United na vilabu vingine (soma hapa)- hapa chini ni sababu tatu kwa nini anaweza kufanya hivyo, kiufupi kuondoka Catalan.

1) Pesa

Muarjentina anazidiwa kimapato na Ronaldo, ambapo bajeti ya mshahara Barcelona inaripotiwa kubanwa kiasi. Hata hivyo England timu kama United, pia Man City au Chelsea wanaweza kutenga pesa ndefu kumpata.

2) Mashitaka ya udanganyifu wa kodi

Messi anadaiwa kutokua na furaha kutokana na mashtaka ya sasa yanayomhusisha na kuchenga kodi Hispania. Wengi wanasema asingekua na matatizo kama haya England kwa sababu ya tofauti ya sheria katika mishahara ya wachezaji na haki ya jina.

3) Suala la kuthibitisha

Kumekuwepo na mijadala kua Messi hawezi kung'aa England. Ni kijana ambaye karibia maisha yake yote ya soka ametumikia Blaugrana, kwa hiyo endapo akihamia kwingine ni wakati wa kuthibitisha kwamba kweli yeye ndiye bora zaidi hata nje ya Barca.


Sababu tatu zinazoweza kumfanya Messi kuondoka Barcelona Sababu tatu zinazoweza kumfanya Messi kuondoka Barcelona Reviewed by Steve on Friday, October 23, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.