Diego Costa adai hajali jinsi gani wengine wanavyomfikiria

'Bad boy' wa Chelsea, Diego Costa amefunguka kua hajali kitu gani watu wanafikiria
kuhusu yeye kama mchezaji na amesema hatoweza kubadilika.
Akiongea kwa mara ya kwanza tangu afungiwe baada ya mechi ya Arsenal mwezi uliopita, Costa amesisitiza kua adhabu haitabadilisha namna anavyocheza ila atabadilika tu endapo bosi wa Blues Jose Mourinho akitaka.
"Nina support y1a 100% kutoka kwa meneja wangu, kutoka kwa klabu na kutoka kwa mashabiki wa Arsenal," aliiambia Daily Mirror.
"Kwa hiyo watu wengine, maoni mengine, sijali. hayanisumbui. Sitabadilika labda meneja au watu wengine kutoka klabuni au wadau wangu wakiniambia.
"Sihitaji kubadilika kwa sababu sina nilichokosea. Katika mpira wangu, mara nyingi wachezaji wengine wamefanya mabaya kwangu, wamenipiga, lakini mimi sio mtoto wa kulia.
"Kwa hiyo nadhani wadau waliona hiyo sio sawa, na kwa hiyo wadau, meneja na klabu wamenipa support kubwa."
...
Pia Mbrazil huyo mzaliwa wa Hispania aliongeza kua haogopi kukaririwa na waamuzi."Sijawahi kuwa na tatizo lolote na maafisa. hakuna kufungiwa kokote kulikotokana na matatizo na maafisa.
"Muda mwingine napewa kadi ya njano. Lakini hiyo ni sehemu ya mchezo, ni kawaida. Nina matumaini kua wananiona tofauti kwa sasa.
"Lakini nadhani wao ni wataalamu zaidi na wataendelea kua hivyo."
Costa amecheza mechi 10 kwa Chelsea msimu huu, akifunga magoli matatu na kusaidia mengine matatu.
Diego Costa adai hajali jinsi gani wengine wanavyomfikiria
Reviewed by Steve
on
Saturday, October 24, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment