Propellerads

Louis van Gaal afafanua kwanini hakumuanzisha Mata dhidi ya CSKA Moscow



                  
Louis van Gaal ameeleza kua uamuzi wake wa kumuacha Juan Mata kwenye
kikosi kilichoanza dhidi ya CSKA Moscow ni kutokana na sababu za 'fitness' kwa nyota huyo.

Akizungumzia maamuzi yake ya kushtukiza kumleta Jesse Lingard kikosi cha kwanza kwenye mechi ya kundi B klabu bingwa jana, Van Gaal amedai alikua na machaguo machache lakini akaishia kufanya hivyo.

"Ninatakiwa nizunguke" aliiambia tovuti rasmi ya Man United. "Juan Mata amecheza karibia kila mchezo. Anahitaji kupumzika kidogo. Siku zote tupo hapa kushinda mpinzani. Wana kasi ya ushambuliaji na natarajia watacheza baada ya mapumziko."

Mechi hiyo Man United walimaliza kwa sare ya 1-1 ugenini mbele ya CSKA Moscow, goli la Man United likifungwa na Antony Martial dakika ya 65, huku wapinzani wao wakipata bao kupitia Doumbia dakika ya 15.
Louis van Gaal afafanua kwanini hakumuanzisha Mata dhidi ya CSKA Moscow Louis van Gaal afafanua kwanini hakumuanzisha Mata dhidi ya CSKA Moscow Reviewed by Steve on Thursday, October 22, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.