Van Gaal hajafurahishwa na kitendo cha kijinga cha Antony Martial
Bosi wa Manchester United, Louis van Gaal amekemea vibaya kwa
ujinga alioufanya Antony Martial kwa kushika mpira ambapo ilipelekea CSKA Moscow kupata goli kwa penati kwenye mechi ya jana ya klabu bingwa ambayo iliisha kwa sare ya 1-1 huko Urusi.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 19 alishika mpira kwenye eneo hatari dakika ya 15 ambapo Seydou Doumbia alimalizia baada ya De Gea kuutema mkwaju wa Roman Eremenko aliyepiga penati hiyo.
Martial alilisahihisha kosa lake baada ya kusawazisha kipindi cha pili,lakini goli lake halijamsahaulisha kocha Mholanzi.
"Kilikua ni kitendo cha kipuuzi kutoka kwa Antony, kabla ya hapo labda ilikua ni Offside , sijui," aliwaambia waandishi.
"Nilidhani ilikua ni offside, lakini sijui. Ilikaribia. Lakini kile kitendo, ni kwa mara ya kwanza anafanya, lakini kwetu ni bahati mbaya kwa sbabu nadhani tuliutawala mchezo.
"Hatukucheza na kasi sana, nadhani. Umiliki wa mpira ulikua taratibu sana kipindi cha kwanza lakini tuliongeza kipindi cha pili na tulifunga goli zuri. Tungeweza kushinda, lakini hiyo hua hatuhesabu kwenye mpira."
Red Devils wanashika nafasi ya pili na CSKA Moscow kundi B, nyuma ya point mbili kwa Wolfsburg.
Van Gaal hajafurahishwa na kitendo cha kijinga cha Antony Martial
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 22, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment