Propellerads

Uthabiti wa Antony Martial wamshangaza Van Gaal


                                        
Bosi wa Manchester United, Louis van Gaal amefunguka kua hata yeye
anashangazwa na kasi aliyonayo Antony Martial katika kuuzoea upepo ndani ya Red Devils.

Mshambuliaji huyo Mfaransa mwenye miaka 19 amefanikiwa kufunga magoli matano katika michuano yote akiwa United tangu awasili toka AS Monaco kwa dau la pauni mil 36.

Japo kocha mdachi anaamini mafanikio yalikua ni swala la kutegemewa, lakini amekiri kua hakutegemea kua kinda huyo kuzoea mapema na kuonesha kiwango cha hali ya juu kwa muda mfupi.

"Sishangazwi nae, hapana, kwa sababu tulimchunguza na kumnunua kutokana na uchunguzi wetu," Van Gaal alisema kama alivyonukuliwa na The Mirror "Kwenye uthabiti, amenishangaza, lakini kuhusu uwezo wake, hapana. Kwa sababu tayari tulijua muda mrefu atafanya hivi.

"Anatakiwa azoee falsafa yetu. Hii ndio point kubwa. Anazoea haraka, lakini anatakiwa azoee na kujiendeleza mwenyewe zaidi. Anaelekea kufanya makubwa.

"Wachezaji chipukizi kawaida hawana msimamo, bado wanaangalia nafasi yao klabuni. Ndio maana nimeomba muda kwa ajili yake. Lakini nimeshasema Antony ni thabiti na mzuri, hata kama bado anaangalia nafasi yake klabuni katika kiwango chake cha mpira."

Martial anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi kitakacho wakaribisha Man City nyumbani Old Trafford jumapili hii.
Uthabiti wa Antony Martial wamshangaza Van Gaal Uthabiti wa Antony Martial wamshangaza Van Gaal Reviewed by Steve on Saturday, October 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.