Messi kuondoka Barca na kujiunga na vilabu hivi Premier League !!

Imeripotiwa kua Lionel Messi ameiambia klabu yake ya sasa ya
Barcelona kua anataka kuondoka ambapo wakubwa wa England Manchester City, Chelsea na Manchester United wanadaiwa kumtengea pesa ndefu ili kumnasa.
Messi amepata kushinda Ballon d'Ors nne akiwa na Barcelona kwa muda wa miaka 11 lakini inasemekana mshambuliaji huyo anataka kujaribu maisha ya England.
Matakwa yake ni ya kimaslahi zaidi ambapo tayari vilabu hivyo vikubwa England tayari inadaiwa vimefanya mazungumzo na wawakilishi wa Messi kwa mujibu wa The Sun.
Mpango wa Messi kuondoka Blaugrana unahusishwa na kesi yake ya kukwepa kulipa kodi Catalunya, ambapo yeye na baba yake Jorge wanakabiliwa na mashtaka ya kukwepa kulipa kiasi kinachofikia pauni mil 3.1
Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kufikia ukomo mwaka 2018
Messi kuondoka Barca na kujiunga na vilabu hivi Premier League !!
Reviewed by Steve
on
Friday, October 23, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment