Propellerads

Yule mchezaji wa Simba aliyebambwa na hirizi huenda akakutana na adhabu hii




                           
Mshambuliaji Msenegali wa Simba, Pape N'daw anaweza kukumbana
na adhabu ya kutozwa faini ya Sh 500,000 kutokana na kuonekana akiwa amevaa hirizi wakati wa mechi kati ya timu yake dhidi ya Prisons kwenye UWanja wa Sokoine, jana.

N'daw alizua tafrani baada ya wachezaji wa Prisons kugundua alikuwa na 'power bank' hiyo na kusababisha mwamuzi kumtoa nje aende akaivue.

Kanuni ya 25, udhibiti wa wachezaji kipengele g(vi)
 kinasema mchezaji atakayejihusisha na masuala ya kishirikina wakati wa mchezo atatozwa faini ya Sh 500,000.

Hata hivyo, majibu ya adhabu, yatategemea kamisaa wa mchezo huo ataandika nini katika ripoti yake na mwamuzi wa akiba aliyeingia chumbani na N'daw wakati aekienda kushusha mzigo huo kilikuwa ni kitu gani.
Yule mchezaji wa Simba aliyebambwa na hirizi huenda akakutana na adhabu hii Yule mchezaji wa Simba aliyebambwa na hirizi huenda akakutana na adhabu hii Reviewed by Steve on Friday, October 23, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.