Van Gaal afichua kibaya zaidi kuhusu Premier League

Bosi wa Manchester United Louis van Gaal amefichua kile
anachoamini kua ni kibaya katika Premier League.
Bosi huyo mdachi hafurahishwi na kutokuwepo kwa mapumziko kipindi cha majira ya baridi England, akifafanua kua timu ya taifa ya England inashindwa kuchukua mataji makubwa kwa sababu wachezaji wake wanachoka sana kila mwisho wa msimu.
"Hamna mapumziko majira ya baridi na nadhani ndio kitu kibaya kwa huu utamaduni," aliviambia vyombo vya habari.
"Sio nzuri kwa mpira wa Uingereza, sio nzuri kwa vilabu au timu ya taifa na nafikiri wanatakiwa waibadilishe.
"England hawajashinda chochote miaka mingapi?
"Ni kwa sababu wachezaji wote wanachoka inapofika mwisho wa msimu."
Van Gaal afichua kibaya zaidi kuhusu Premier League
Reviewed by Steve
on
Friday, October 23, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment