Propellerads

Messi afichua siri iliyopo kati ya uhusiano wake na Cristiano Ronaldo


                           

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanaonekana kua mahasimu
wakubwa katika soka, lakini muarjentina sasa amefichua ukweli uliopo katika uhusiano wake yeye na nyota mreno.

Wawili hao wameshinda ballon d'Or saba zilizopita kati yao huku wakijitahidi kila mmoja kua bora zaidi.

Hata hivyo, Messi sasa amefafanua kwamba amelenga pekee katika timu anayoichezea na sio kushindana na Ronaldo.

"Kuna vitu watu wanasema. Sishindani na Cristiano na yeye hatakiwi kushindana na mimi" alimwambia mchambuzi wa kihispania Guillem Balague wakati alipofanya interview na Yahoo Sport.

"Ninachokitaka ni mazuri kwa timu yangu na ndicho ninachokifanyia kazi ."

Nyota huyo pia aligusia jeraha lake akieleza kua anaelekea kupona.

"Ninapata maendeleo siku hadi siku" alimaliza Messi.
Messi afichua siri iliyopo kati ya uhusiano wake na Cristiano Ronaldo Messi afichua siri iliyopo kati ya uhusiano wake na Cristiano Ronaldo Reviewed by Steve on Friday, October 23, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.