Propellerads

Endapo Mourinho akitimuliwa, Brendan Rodgers kuifundisha Chelsea!!

                     

Aliyekua kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers ameripotiwa kua huenda
akawa kocha wa muda wa Chelsea endapo mabingwa hao wa Premier League wataamua kuachana na Jose Mourinho.

Rodgers mpaka sasa hana timu yoyote tangu afukuzwe kuinoa Liverpool Oktoba 4 mwaka huu baada ya kufundisha miaka mitatu bila taji lolote  Anfield.

Nafasi ya Mourinho kwa sasa iko katika msukumo mkubwa baada ya kushinda michezo mitatu pekee ya ligi kati ya 10 pia migogoro ya mara kwa mara na chama cha soka.

Kwa mujibu wa Belfast Telegraph, kama ikitokea Mourinho akioneshwa mlango wa kutokea, Rodgers atashika majukumu The Blues kama kocha wa muda huku klabu ikitafuta kocha wa kudumu.

Rodgers alifanya kazi kama kocha wa vijana na kikosi cha reserve Chelsea kipindi cha kwanza kabisa Mourinho kuinoa timu hiyo kati ya mwaka 2004 na 2007.

The Blues ambao kwa sasa wako nafasi ya 15 wanaumana na Liverpool leo jumamosi.
Endapo Mourinho akitimuliwa, Brendan Rodgers kuifundisha Chelsea!! Endapo Mourinho akitimuliwa, Brendan Rodgers kuifundisha Chelsea!! Reviewed by Steve on Saturday, October 31, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.