Jose Mourinho hana hofu na kibarua chake

Kocha wa Chelsea aliye katika wakati mgumu kwa sasa, Jose Mourinho amesisitiza kua hajali sana
hali ilivyo sasa na hatma yake Chelsea.
Kocha huyo mwenye miaka 52 imeripotiwa kua huenda akatimuliwa endapo Chelsea itapoteza mbele ya Liverpool leo jumamosi, huku mabingwa hao wa Premier League wakiwa nyuma ya point 11 kwa vinara Man City na Arsenal kufuatia mwanzo mbaya kabisa wa msimu katika kipindi cha miaka 38.
Pamoja na yote, Mourinho ambaye amekaa nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi, amefunguka kua ana wasi wasi na matokeo yajayo ya timu na sio kibarua chake.
"Sina wasi wasi na kazi yangu. Sina wasi wasi na hatma yangu," alisema kama alivyonukuliwa na Sky Sports News "Situmii hata sekunde yangu moja kwa siku kufikiria kuhusu hilo.
"Inaonekana unataka kuweka pressure kubwa kwangu kuhusiana na hilo, ambapo huwezi kufanya hivyo. Huwezi kufanya hivyo. Nina wasi wasi na matokeo. Nina wasi wasi na kushinda (leo jumamosi). Nina was wasi na kufuzu hatua inayofuata Champions League.
"Nina wasi wasi na kurudisha nafasi katika msimamo na kuiweka Chelsea ilipozoeleka kua."
Chelsea wamepoteza michezo nane kati ya 16 waliyocheza mpaka sasa katika michuano yote msimu huu.
Jose Mourinho hana hofu na kibarua chake
Reviewed by Steve
on
Saturday, October 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, October 31, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment