Hili jipya kutoka Chelsea kuhusu Mourinho

Imeripotiwa kua Jose Mourinho bado amepewa muda kuhakikisha mambo
yanaenda kwenye mstari klabuni Chelsea pamoja na kwamba timu yake imepoteza mchezo wa saba sasa katika Premier League.
Kocha huyo Mreno hakuepo wakati timu yake ilipopoteza kwa 1-0 mbele ya Stoke City baada ya kupewa adhabu ya kufungiwa mechi moja.
Mourinho ambaye amekua na visa vya mara kwa mara na chama cha soka cha England msimu huu, alifungiwa baada ya kukwaruzana na mwamuzi Jonathan Moss kwenye mechi dhidi ya West Ham ambapo nayo walipoteza kwa 2-1.
Huku baadhi ya ripoti zikidai kua sasa Mourinho huenda akaondoka, Daily Star wao wamedai kua mmiliki wa klabu, Roman Abramovich yupo tayari kumpa muda zaidi kocha huyo kubadilisha hali ya sasa.
Chelsea kwa sasa wako nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi, ikiwa ni point tatu pekee kutoka mstari mwekundu mwishoni.
Hili jipya kutoka Chelsea kuhusu Mourinho
Reviewed by Steve
on
Tuesday, November 10, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, November 10, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment