Wakala wa Ronaldo azungumzia Ronaldo kurejea Man United, je ni kweli yuko tayari!!

Wakala wa Cristiano Ronaldo, amefichua kua nyota huyo bado anaipenda
Manchester United lakini sio sababu ya yeye kumfanya arejee tena Old Trafford.
Hivi karibuni Ronaldo alidokeza kua siku moja anaweza kujiunga tena na klabu aliyoondoka mwaka 2009 baada ya kutimkia kwa wakali wa Hispania kwa uhamisho uliovunja rekodi.
Alipoulizwa kuhusu Premier League ndani ya kipande cha filamu inayozungumzia maisha yake , Ronaldo alinukuliwa na The Mirror akisema "Kwanini isiwe? Sasa hivi nipo La Liga Hispania. Lakini kama nilivyosema mara 100, baadae, hakuna anayejua."
Wakala wake, Jorge Mendes anatarajia Mreno huyo kukaa Bernabeu kwa kipindi chake cha kucheza soka kilichobakia akisema "Nadhani atamalizia kazi yake Real Madrid.
"Nina uhakika, anaipenda Manchester United, anaipenda Madrid. Kwa sasa anaichezea Real Madrid, na tamalizia kazi yake Real Madrid."
Ronaldo amekua ni mfungaji bora wa muda wote Real Madrid tangu ajiunge na klabu hiyo miaka sita iliyopita.
Wakala wa Ronaldo azungumzia Ronaldo kurejea Man United, je ni kweli yuko tayari!!
Reviewed by Steve
on
Tuesday, November 10, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, November 10, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment