Ancelotti kuchukua mikoba ya Mourinho, mwenyewe ana hili la kusema


Kocha mkongwe, Carlo Ancelotti anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi
ya Jose Mourinho amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema, wachezaji Chelsea ndiyo tatizo.
Ancelotti amekiri anegpenda kufanya kazi England, lakini akasisitiza, Mourinho hana kosa kama wachezaji watashindwa kujihamasisha wao binafasi.
“Kweli wachezaji wanapaswa kuhamasishwa, hii ni kazi ya kocha. Lakini Mourinho hawezi kufanikiwa kama wachezaji watashindwa kujihamasisha wao wenyewe.
“Naona kama msimu uliopita Chelsea walichukua ubingwa kiulauni sana. Huenda msimu huu suala la uhamasishaji halikupewa nafasi. Lakini katika hili la kufanya vibaya, wachezaji hawawezi kujiweka kando,” Ancelotti aliliambia Sportsmail la Uingereza.
“Pamoja na yote, katika soka wakati mwingine yanatokea mambo, hauwezi hata ukaelezea. Kumbuka Istambul nikiwa AC Milan, hadi mapumziko tulikuwa mbele kwa mabao 3-0. Lakini kipindi cha pili tukaruhusu mabao matatu, ikawa sare na mwisho Liverpool wakachukua kombe.”
Ancelotti kuchukua mikoba ya Mourinho, mwenyewe ana hili la kusema
Reviewed by Steve
on
Thursday, November 12, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, November 12, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment