Ronaldo: Lionel Messi atanishinda kwenye Ballon d'Or

Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunguka kua anatarajia
hasimu wake Lionel Messi 'atamfunika' kwenye tuzo ya Ballon d'Or mwezi Januari.
Ronaldo, alifunga magoli 61 kwenye msimu wa 2014-15 ambao yeye anadai huenda ukawa ni msimu bora zaidi katika kipindi chake katika mafanikio binafsi.
Hata hivyo, Messi naye ametupia magoli 58 na kuisaidia Barcelona kushinda 'treble' msimu uliopita na sasa Cr7 ambaye ameshinda mara tatu, anatarajia hasimu wake kubeba ushindi kwa mara ya tano.
"Kiukweli, nadhani Messi anaenda kushinda mwaka huu hii tuzo, inategemea kura," aliiambia ITV wakati alipokua kwenye interview na mwandaaji Jonathan Ross.
"Umeshinda michuano mbali mbali, umeshinda klabu bingwa, umeshinda ligi.
"Nilikua na msimu ambao unaelekea ulikua ni mzuri kwangu, na nilikua mfungaji zaidi Ulaya lakini yote inategemea kura, ni ngumu na kiukweli sina shaka na hilo kwa sababu kama nilivyosema mara nyingi, sikuwahi kutarajia kushinda mara tatu kiukweli."
Ronaldo: Lionel Messi atanishinda kwenye Ballon d'Or
Reviewed by Steve
on
Friday, November 13, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, November 13, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment