Propellerads

Habari ya De Bruyne na Man United imefikia hapa



Taarifa zilizoripotiwa zinasema kua kumbe Man United
hawajaweka dau lolote kwa nyota wa Wolfsburg Kelvin De Bruyne.

Mahasimu wa United, Man City wanadaiwa kua karibu kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo kwa ada ya  £50million ambayo imekubaliwa.

Hata hivyo, hivi karibuni uliibuka uvumi ukisema Louis van Gaal anataka kuingilia dili hilo la De Bruyne.

Lakini Sky Sports wameripoti kua Man United hawajaweka dau lolote kwa nyota wa zamani wa Chelsea.

Kwa upande mwingine Bayern Munich nao wamedaiwa kuonesha nia yao, huku Rais wa klabu hiyo Karl-Heinz Rummenigge amekua akijaribu kuangalia namna ya kuipata saini hiyo.

Man City sasa ndio wanaonekana kua mbele kwenye dili hilo ambapo wanatarajiwa kumleta klabuni muda wowote kwa dau linlokadiriwa kua zaidi ya pauni mil 50.
Habari ya De Bruyne na Man United imefikia hapa Habari ya De Bruyne na Man United imefikia hapa Reviewed by Steve on Wednesday, August 26, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.