Propellerads

Tetesi za Usajili Ulaya; Arsenal mbioni kumsajili mshambuliaji kutoka Dynamo Moscow



Klabu ya Arsenal wameripotiwa kua katika harakati za
kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka Dynamo Moscow, Alexander Kokorin.

Gazeti la Daily Star limeripoti kua kocha Arsene Wenger anataka kumshawishi mchezaji huyo akubali kutua The Gunners.

Kokorin ambaye ni miongoni mwa washambuliaji hatari zaidi Urusi, anatajwa kua katika rada za vilabu vingine pia kama vile Paris St-Germain, Manchester United na Zenit St Petersburg.

Tayari wakala wa mshambuliaji huyo amekaririwa akisema kua analifanyia swala la kumpeleka mchezaji wake Premier League, lakini hakueleza ni klabu gani haswa.
Tetesi za Usajili Ulaya; Arsenal mbioni kumsajili mshambuliaji kutoka Dynamo Moscow Tetesi za Usajili Ulaya; Arsenal mbioni kumsajili mshambuliaji kutoka Dynamo Moscow Reviewed by Steve on Wednesday, August 26, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.