Propellerads

Mazoezi ya Stars: Kina Msuva, Mandawa watisha zaidi!



KIKOSI cha Taifa Stars kimeendelea jana na mazoezi kwenye
mji mdogo wa Kartepe huku Kocha Boniface Mkwasa akianza na mazoezi ya kukimbia kasi.

Wachezaji wa Stars walifanya mazoezi ya kukimbia kwa kasi na Simon Msuva, John Bocco na Rashind Mandawa wakiibuka kidede huku wakijisifia kwamba wana kasi kama ile ya mwanariadha maarufu wa Jamaica, Hussein Bolt.
Akisaidiana na msaidizi wake, Hemed Morocco, Mkwasa alikuwa akiwapa nafasi ya kukimbia kwa kasi kubwa ndani ya Mita 100.

Mara kadhaa, Msuva aliyekuwa akijisifia kuisaka kasi ya Bolt ndiye alikuwa akiongoza katika kundi lake.

Bocco na Mandawa, kila mmoja aliongoza kundi lake na ndiyo waliofanikiwa kumaliza kwa sekundu 10 hadi 11.

Pamoja na mazoezi hayo ya kasi, pia walipata nafasi ya kuuchezea mpira, halafu Mkwasa akawapunguza na kugawa timu zenye watu watano watano.

Mazoezi hayo ya kama saa mbili na nusu yalimalizika saa sita kasorobo na wachezaji walipata muda wa kupumzika kabla ya kula chakula cha saa saba na nusu na saa 10 jioni wakarejea mazoezini.

Mazoezi ya Stars: Kina Msuva, Mandawa watisha zaidi! Mazoezi ya Stars: Kina Msuva, Mandawa watisha zaidi! Reviewed by Steve on Wednesday, August 26, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.