Propellerads

Taarifa kutoka Rais wa Barca kuhusu dili la Neymar na Man United



Rais wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amekanusha
uvumi ulioenea kuhusu Neymar kuhamia Man United, ambapo amesema kua nyota huyo lazima astaafie kwa wakali hao wa Hispania.

Red Devils wameripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari hivi karibuni kua wametenga dau linalofikia €190 million  ili kuipata saini ya mbrazili huyo.

Hata hivyo, Bartomeu amesema kua hawako tayari kumpoteza Neymar na wanataka achezee klabu hiyo katika maisha yake yote ya soka.

"Hatutaki Neymar aondoke" aliiambia Radio Catalunya.

"Bado ni kijana na tunataka mpaka astaafie hapa.

"Tutazungumzia kuongeza mkataba baadae mwezi huu, anaweza kukaa hapa sio kwa misimu mitatu tu ijayo, bali hata mitano kabisa au kumi ijayo"

Neymar alikua katika kiwango kizuri msimu uliopita, ambapo alicheza mechi 51 na kufunga magoli 39.




Taarifa kutoka Rais wa Barca kuhusu dili la Neymar na Man United Taarifa kutoka Rais wa Barca kuhusu dili la Neymar na Man United Reviewed by Steve on Wednesday, August 26, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.