Swala la msenegal wa Simba halijampita Julio, nae ameongea yake
Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wachezaji
wengi wengi wa kigeni wanaokuja kucheza soka la kulipwa Tanzania wanauwezo wa kawaida ukilinganisha na sifa ambazo wanakuwa wakipewa.
Julio ametoa kauli hiyo siku mbili baada ya kucheza mcezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Simba ambayo iliutumia mchezo huo kumjaribu mchezaji wa kigeni Papa Niang kutoka Senegal ambaye kiwango chake kilikuwa ni cha kawaida kwa mujibu wa Julio.
“Mimi nilishasema, zamani kwamba hawa wacheaji wageni wakawaida tu sawa na wa hapa kwetu lakini magazeti yanawaandika sana laiki matokeo yake hawana kiwango wanachokionesha. Walisema kunamchezaji mdogowake Mamadou Niang lakini ukimwangalia uwezo wake na sifa alizopewa mara mtambo wa magoli, mara anauwezo mkubwa lakini alichokifanya mimi sijui”, amesema Julio.
“Ukiniambia nimchague mchezaji bora kwa ile mechi mechi yetu, basi bila shaka ntakutajia Mwinyi Kazimoto na Awadh Juma”.
“Sasa tukiwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kama hao, sasa hawa kina Niang wanini, tuache mambo ya kuiga na kushikilia kuwa wachezaji wa kimataifa wanauwezo mkubwa kuliko watoto wetu. Mimi siamini kama mchezaji kutoka nje hata Senegal anaweza kuja kucheza professional football Tanzania, sasa mbona huyo Mamadou Niang hakuja”.
“Nilishasema Pascal Wawa ni moja ya wachezaji waliokuja hapa kikazi zadidi, kuna mtu kama Kipre Tchetche, Okwi, Haruna Niyonzima hao ndio maprofessional lakini wengine wapowapo tu lakini wanachofanya hakuna hawana tofauti na wachezaji wetu tena wachezaji wetu wanauwezo mkubwa”.
Swala la msenegal wa Simba halijampita Julio, nae ameongea yake
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 26, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment