Mbali na Neymar,Mbrazili mwingine tena ahusishwa na Man United
Mchezaji wa zamani wa AC Milan na timu ya taifa ya Brazili,
Alexandre Pato amehusishwa na kutaka kuhamia Man United.
Man United wamekua wakihusishwa na wachezaji wengi msimu huu wa usajili, lakini taarifa za kushtukiza kutoka The Telegraph zinadai Man United wako katika mazungumzo na mbrazil huyo.
Ripoti imeeleza kua Pato ambaye anachezea Sao Paulo ya Brazil amekua akifukuziwa na vilabu vingi vya Uingereza ikiwemo United na Chelsea.
Mshambuliaji huyo anaweza kupatikana kwa kiasi cha £10.9 million, ambapo imeelezwa kua yuko tayari kurejea kwenye soka la Ulaya.
Akiwa na miaka 25 sasa, Pato alikua anatajwa sana kua ni miongoni mwa vipaji vinavyokuja kwa kasi zaidi Ulaya, lakini bahati mbaya majeraha ya muda mrefu yalikwamisha maendeleo yake.
Akiwa AC Milan pato amepata kufunga magoli 63 katika mechi 150 alizocheza, na kama dili hili likiwa kweli Pato anatarajiwa kuongeza nguvu kubwa ya ushambuliaji Man United.
Mbali na Neymar,Mbrazili mwingine tena ahusishwa na Man United
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 25, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment