Propellerads

Kuhusu Msenegal, Matola aongelea tahmini ya benchi la ufundi la Simba




Kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema, benchi la
ufundi la timu hiyo bado linamfanyia tathmini mchezaji wa kigeni Papa Niang anaefanya majaribio kwenye klabu hiyo. Matola ameongeza kuwa, ligi ya msimu ujao itakuwa ngumu kutokana na timu zote kufanya maandalizi ya kutosha.

Simba jana ilicheza mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga na timu hizo kutoka sare ya bila kufungana lakini Simba wakiwa wamepteza nafasi nyingi za kufunga magoli huku Niang akionekana ni wa kiwango cha kawaida na sio kama ilivyokuwa inadaiwa.

“Kuhusu mshambuliaji mpya, huyu bado tunaendelea kumfanyia tathmini. Ukiangalia Niang kaja anaonekana kabisa hakuwa akifanya wazoezi, hayuko fiti, bado tunamuda wa kufanya tathmini na tutatoa majibu”, amesema Matola.

“Tuliweza kucheza vizuri, tulitengeneza nafasi lakini hatukuzitumia vizuri. Naamini ligi itakuwa ngumu kwasababu timu zote zimejiandaa vizuri lakini yote kwa yote lazima ujiandae kukabiliana na ugumu wa ligi”.

“Unapofanya makosa halafu unamuda, unapata nafasi ya kurekebisha makosa yako zimebakia kama wiki mbili hivi kabla ya ligi kuanza, kweli tumetengeneza nafasi lakini goli zimekosekeana kwavile bado tuna wiki mbili tunaweza kurekebisha makosa yale ambayo tumeyaona ili tuweze kufanya vizuri kwenye ligi inayokuja”.

“Nafikiri tutakuwa na mechi tena mwishoni mwa juma hili nadhani baada ya mechi hiyo tutatoa tahmini ya wachezaji ambao tukonao”.
Kuhusu Msenegal, Matola aongelea tahmini ya benchi la ufundi la Simba Kuhusu Msenegal, Matola aongelea tahmini ya benchi la ufundi la Simba Reviewed by Steve on Tuesday, August 25, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.