Propellerads

Baada ya kuchemsha jana, Msenegal wa Simba ajitetea namna hii



Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba anaefanya majaribio kwenye
timu hiyo, Papa Niang jana ameshindwa kuonesha makali yake kwenye mchezo wa kirafiki wakati Simba ikicheza dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Niang aliyeanza kwenye kikosi cha Simba kilichoanza kwenye mechi hiyo amekiri kuwa hakuwa kwenye kiwango kizuri lakini akatoa sababu za kwa nini amecheza chini ya kiwango tofauti na matarajio ya mashabiki wengi wa Simba.

Akizungumza na mtandao wa Shaffihdauda Niang amesema, alikuwa kwenye mapumziko kwa muda mrefu kwahiyo ‘ufiti’ wake umepungua kwa kiasi kikubwa na tangu amewasili Simba amefanya mazoezi kwa siku mbili na kikosi hicho hivyo anahitaji apate muda wa kuzoeana na wachezaji wa timu hiyo pamoja na aina ya soka la wakali hao wa Msimbazi.

“Ni kweli sijaonesha kiwango kizuri kwasababu nimetoka likizo, na kila sehemu unapokwenda unahitaji muda ili kuzoea, mimi najaribu kuzoea mpira wa Simba. Sifahamiani na wachezaji, nimefanyanao mazoezi kwa siku mbili na leo tulikuwa na mechi kwahiyo nilikuwa najaribu kuendana na mfumo wao”, amesema Niang.

“Kilamahali unapokwenda inabidi ujitahidi kuendana na aina ya soka lao, lakini naamini kabla ya ligi kuanza nitakuwa nimeshazoea na nitaonesha ubora wangu”.

“Mechi ilikuwa nzuri timu zote zilijaribu kucheza mchezo mzuri, nimefurahishwa sana na mchezo wa leo”.

Baada ya kuchemsha jana, Msenegal wa Simba ajitetea namna hii Baada ya kuchemsha jana, Msenegal wa Simba ajitetea namna hii Reviewed by Steve on Tuesday, August 25, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.