Propellerads

Kiongozi wa juu Man United aenda hispania kukamilisha dili la Pedro


Pedro

MTENDAJI mkuu wa klabu ya Manchester United, Ed Woodward amepaa
kwa ndege hadi Barcelona kukamilisha dili la Pedro ambalo litagharimu kiasi cha £22m.

Kwa taarifa zaidi like page yetu ya facebook hapa

Pamoja na klabu kuwa na mchezo kwa ajili ya michuano ya UEFA dhidi ya klabu ya Bruges ya Ubelgiji utakaopigwa Old Trafford, Woodard amesafiri hadi hispania kumsajili winga huyo.

Kocha wa Man United, Louis van Gaal anataka kuongeza ufundi na magoli zaidi kikosini huku Pedro ambaye amewekewa ofa hiyo ya pauni 22m akionekana kutaka kuachana na mabingwa wa Ulaya Barcelona kutokana na malalamiko yake ya kutopata muda wa kutosha kucheza uwanjani.

Kitu kingine ambacho Ronaldo yuko juu ya nyota wengine

Pedro alitokea benchi kwenye mechi ya fainali ya Super Cup dhidi ya Sevilla wiki iliyopita hali iliyopelekea akakasirika kwanini hakuanza kikosi cha kwanza ilhali Neymar hakuwepo kutokana na maradhi.

Bosi wa Barca Luis Enrique bado anataka kuendelea na nyota huyo, lakini amesisitiza kua maamuzi yote yako kwa Pedro mwenyewe.


Kiongozi wa juu Man United aenda hispania kukamilisha dili la Pedro Kiongozi wa juu Man United aenda hispania kukamilisha dili la Pedro Reviewed by Steve on Tuesday, August 18, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.