Maafisa wa Chelsea wasafiri hadi Italia kumsainisha 'Essien mpya'
Maofisa wa klabu ya Chelsea wamesafiri hadi Italia kumsainisha
nyota Godfred Donsah.
Mchezaji huyo mwenye miaka 19 ni miongoni mwa walio katika mahesabu ya kocha Jose Mourinho ambaye ameanza vibaya msimu huu.
Chelsea wana pointi moja pekee katika michezo miwili ya mwanzo huku tayari mipasuko ikianza kuonekana.
Iko wazi kocha Mourinho anajipanga kukimarisha zaidi kikosi chake kwa kumnasa Donsah.
Mchezaji huyo wa Cagliari mzaliwa wa Ghana alihamia Italy mwaka 2012 na kujiunga na Palermo kabla ya kuelekea Verona kwa mkopo.
Kuhamia kwake Chelsea wengi wanamuita 'Essien mpya'
Maafisa wa Chelsea wasafiri hadi Italia kumsainisha 'Essien mpya'
Reviewed by Steve
on
Monday, August 17, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 17, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment