Inaweza kuwa kweli??!!, Muller amewaambia rafiki zake anataka Man United
anataka kujiunga Man United majira haya ya kiangazi, hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Express.
Katika majira haya ya joto, Muller amekua akihusishwa sana kutaka kuhamia Old Trafford, lakini hata hivyo tayari ofa mbili za kocha Louis van Gaal zimekataliwa na Bayern Munich. Ofa ya mwisho ilidaiwa kufikia £60 million.
Taarifa hii inaweza kua nzuri zaidi upande wa Red Devils kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi huu.
The Express wamedai kua Muller ameweka wazi maamuzi yake binafsi kwa rafiki zake, huenda akavunja rekodi ya usajili , lakini haya yote yataeleka tu mpaka kufikia kufungwa kwa dirisha la usajili.
Muller alikua katika kiwango kizuri zaidi msimu uliopita, akiifungia Bayern magoli 13 katika mechi 32 za ligi, lakini hata hivyo alicheza mpaka dakika 90 katika mechi 14 pekee.
Inaweza kuwa kweli??!!, Muller amewaambia rafiki zake anataka Man United
Reviewed by Steve
on
Monday, August 17, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 17, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment