Propellerads

Hatimaye Manji arejeshwa kugombea udiwani Mbagala kuu



Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf manji amerudishwa katika nafasi yake ya
kuwania udiwani katika kata ya Mbagala Kuu.

Manji alishinda kwa kishindo, lakini akaenguliwa katika hali iliyoelezwa kuwa ya figisufigisu.

Umeipata hii!!, Manji nae amekatwa jina lake udiwani Mbagala Kuu

Hata hivyo, KAmati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi iliyokaa jana, imemrejesha Manji baada ya wahusika kukimbia wakati wa kuhojiwa.

“Ulipofika wakati wa wahusika kuhojiwa, hawakuwepo, walipopigiwa simu walikuwa wamechelewa na kusema wanakuja lakini baada ya muda walizima simu.

“Hali hiyo ilifanya kamati kuu moja kwa moja kuchukua uamuzi wa kumrejesha Manji katika nafasi yake aliyoshinda kwa kishindo,” kilieleza chanzo.


Wananchi wa Mbagala Kuu walionyesha hasira zao kwa kuvamia makao makuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakitaka Manji arudishwe baada ya kugundua aliondolewa kwa fitita licha ya ushindi wake wa kishindo.
Hatimaye Manji arejeshwa kugombea udiwani Mbagala kuu Hatimaye Manji arejeshwa kugombea udiwani Mbagala kuu Reviewed by Steve on Thursday, August 20, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.