Propellerads

Umeipata hii!!, Manji nae amekatwa jina lake udiwani Mbagala Kuu


Manji akiwasi kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Jina la Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji limeenguliwa kwenye kinyang’anyiro
cha kuwania Udiwani Kata ya Mbagala Kuu huku ikidaiwa kuwepo kwa mchezo mchafu ‘figisufigisu’ katika ‘kulikata’ jina Manji ambaye alishinda kwa kishindo kwenye kura za maoni kuteuliwa na chama chake cha CM kugombea nafasi hiyo kwenye kata ya Mbagala Kuu.

Manji (katikati) akiingia kwenye lango la ofisi za Mkoa

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo walijazana kwenye ofisi ya mkoa wa Dar es Salaa ya chama hicho wakipinga kuenguliwa kwa mgombea wa nafasi ya Udiwani Kata ya Mbagala kuu Bw. Yusuf Manji huku wakitaka ufafanuzi wa kina sababu zilizotumika kuliondoa jina la Manji kugombea nafasi ya Udiwani.

Wanachama wa CCM ambao ni wakazi wa kata ya Mbagala Kuu wakiwa kwenye ofisi za chama hicho mkoa wa Dar es Salaam wakisubiri hatma ya Manji

Baada ya muda mfupi tangu mtandao huu upige kambi yake kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Manji akiwa katika hali ya udhoofu aliwasili akiwa na bahasha mkononi inayosemekana ni barua ya kupinga maamuzi yaliyotolewa ya kuliondoa jina lake kwenye kinyang’anyiro hicho.

Manji 11

Mtandao huu ulijaribu kufanya mazungumzo na Manji lakini alidai hayuko katika hali yake ya kawaida kutokana na kusumbuliwa na maradhi hivyo hayupo tayari kuzungumza chochote kwa muda huo na kuomba akimilishe kile kilichompeleka kwenye ofisi za CMM Mkoa.

Manji 6

Baada ya zoezi la kuzungumza na Manji kukwama, mtandao huu ukaona ni vyema kuzungumza na baadhi ya wanachama ambao walikuwa wamepiga kambi kwenye ofisi hizo kusubiri hatma ya mgombea wanaedai ndiye chaguo lao.

Manji 10

Victor Chitete amehusisha kukatwa kwa jina la manji na siasa za Simba na Yanga kutokana na baadhi ya viopngozi wa juu wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni mashabiki, wanachama na wanazi wa Simba ambao ni watani wa jadi wa Yanga.

“Kuna viongozi wa nafasi za juu kwenye chama ngazi ya mkoa ambao wanafanya kila liwezekanalo ili kuzuia Manji asipite kwenye nafasi ya Udiwani anayogombea kwasababu ya siasa za Simba na Yanga kwasababu wao ni viongozi wa klabu ya Simba”.

Manji

Shabani Dotto Kadala yeye ni mwanachama wa CCM na mkazi wa Kata ya Mbagala Kuu amesema, Manji ni mtu makini na wanaimani nae kutokana na uwezo wake aliouonesha wa kuiongoza klabu ya Yanga yenye mamilioni ya washabiki na kumudu kuiongoza kwa utulivu bila migogoro kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.

“Manji ni mtu makini na ni mtekelezaji, amethibitisha hilo akiwa Yanga. Ninavyoiangalia Yanga haina mjadala kwamba Manji ni mchapakazi na ni mtendaji. Ameweza kutoa ajira nyingi kupitia Yanga wengine wakiwa ni wadogozetu. Kupitia hilo sisi hatuna mashaka nae”, amesema Kadala.

Manji 7

“Tumekuja kufikisha ujumbe kwamba tunamuhitaji mgombea wetu bwana Yusuf Manji ambaye tulimpitisha kwenye kura za maoni na kuna tetesi kwamba jina lake limekatwa. Taarifa hizi tumezipata kwa viongozi wetu na baadhi ya wanachama wa CCM wa Mbagala Kuu, walitueleza kwamba kiongozi wetu jina lake limekatwa”.

Manji 5

“Tumefika hapa katibu mwenezi wa mkoa wa Dar es Salaam ametuhakikishia kuwa jina la Manji limekatwa na ametupa sababu kadhaa ambazo wanadai hakuwahi kuhudhuria kwenye baadhi ya vikao vya kuomba kura za maoni na kutangaza kura zake. Wanadai viongozi wa Kata na Wilaya walimuita hakufika kitu ambacho si kweli. Sisi wanachama tulionananae akatueleza sera zake tukavutiwa nazo tuka mchagua”.

SOURCE: Mtandao wa Shaffihdauda.com

Umeipata hii!!, Manji nae amekatwa jina lake udiwani Mbagala Kuu Umeipata hii!!, Manji nae amekatwa jina lake udiwani Mbagala Kuu Reviewed by Steve on Sunday, August 16, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.