Propellerads

Kwanini Pedro alipendelea ofa ya Chelsea na sio Manchester, sababu yaelezwa



Manchester United walishindwa kumsajili nyota wa Barca, Pedro ambaye
kwa sasa anaelekea Chelsea, imeelezwa kua yeye mwenyewe alipendelea The Blues zaidi.

Inadaiwa wachezaji wenzie wawili aliokua nao Barcelona ndio waliomshawishi kwa kiasi kikubwa kuchagua Chelsea kuliko Man United.

Unyanyasaji aliokua nao kocha Louis van Gaal kwa kipa Victor Valdes imedaiwa kuchangia maamuzi ya nyota huyo pia uwepo wa Cesc Fabregas klabuni Chelsea imetajwa kua sababu nyingine.

Kwa sasa tayari Pedro ameripotiwa kuelekea London kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho huku uhamisho wake ukitarajiwa kutangazwa muda wowote.
Kwanini Pedro alipendelea ofa ya Chelsea na sio Manchester, sababu yaelezwa Kwanini Pedro alipendelea ofa ya Chelsea na sio Manchester, sababu yaelezwa Reviewed by Steve on Thursday, August 20, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.