Propellerads

Tambwe anaweza asicheze mechi ya Mtibwa, huenda Mzenji akaziba nafasi yake, vipi kuhusu Chirwa!? cheki hapa



Kuna hatari ya Yanga kucheza bila ya mshambuliaji wake
Amissi Tambwe kesho Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar katika Ligi kuu bara kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Kutokana na hali hiyo, Yanga tangu juzi Alhamisi ilianza kumuandaa mshambuliaji wake Emmanuel Martin ili acheze nafasi ya Tambwe ambaye ni majeruhi wa goti.

Tambwe anatarajiwa kuukosa mchezo huo baada ya kujitonesha goti lake katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting Jumatano iliyopita uwanja wa Taifa Dar.

Habari kutoka benchi la ufundi la Yanga zinasema Emmanuel atachukua nafasi ya Tambwe na Juma Mahadhi anaweza kucheza nafasi ya Obrey Chirwa ambaye hana uhakika wa kucheza kwani rufaa yake ya kadi nyekundu inasikilizwa leo Jumamosi na kamati ya masaa 72.

"Kama unavyoona kikosi chetu kinaandamwa na majeruhi na wachezaji wenye adhabu ya kadi, hivyo benchi la Ufundi linatumia akili kukiandaa kikosi chetu ili kipate matokeo mazuri licha ya matatizo hayo.

"Hii ni mechi ngumu kwetu ndiyo maana tunapambana, hivyo Emmanuel na Mahadhi watacheza katika nafasi za Tambwe na Chirwa kama hakutatokea mabadiliko." kilisema chanzo cha taarifa.
Tambwe anaweza asicheze mechi ya Mtibwa, huenda Mzenji akaziba nafasi yake, vipi kuhusu Chirwa!? cheki hapa Tambwe anaweza asicheze mechi ya Mtibwa, huenda Mzenji akaziba nafasi yake, vipi kuhusu Chirwa!? cheki hapa Reviewed by Steve on Saturday, March 04, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.