Propellerads

Mayanja ana msimamo huu kuhusu ubingwa baada ya sare na Mbeya City



Kocha msaidizi wa kikosi cha Simba Jackson Mayanja amefunguka kwamba bado kuna uwazi katika mbio za kuwania ubingwa  kwa timu zinazowania ubingwa huo msimu huu ambazo ni Simba na Yanga. Mayanja ameyasema hayo kufuatia Simba kupata sare ya magoli 2-2 na Mbeya City uwanja wa taifa Dar es Salaam.
“Hii inaonesha ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom bado ni mgumu, hatujui nini kitatokea kwa Yanga ambao ndio tunawania nao ubingwa nab ado pia watacheza na Azam. Mimi sitaki kuzungumzia  sana kuhusu Yanga, sisi tunaangalia mechi zetu kama tunaweza kushinda zote zilizobaki,” Jackson Mayanja.
Endapo Simba ingeshinda mchezo wake huo wa nyumbani dhidi ya Mbeya City, ingepaa na kufikisha pointi 57 na kuongeza wigo mpana zaidi ya wapinzani wao Yanga ambao leo Jumapili wanatarajiwa kuumana na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Yanga wakishinda mchezo wao dhidi ya Mtibwa watafikisha pointi 55 sawa na Simba na wataongoza ligi kwa tofauti ya wastani wa magoli.
Mayanja ana msimamo huu kuhusu ubingwa baada ya sare na Mbeya City Mayanja ana msimamo huu  kuhusu ubingwa baada ya sare na Mbeya City Reviewed by Steve on Sunday, March 05, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.